ALICHOKISEMA CONTE KUELEKEA ARSENAL vs CHELSEA - Darajani 1905

ALICHOKISEMA CONTE KUELEKEA ARSENAL vs CHELSEA

Share This
Kama ilivyo kawaida ya kocha Antonio Conte kufanya mkutano na waandishi wa habari siku moja kabla ya mchezo ambao Chelsea itashuka kucheza wiki hiyo. Leo tena amefanya mkutano kuelekea mchezo wa kesho kati ya Chelsea itakapokaribishwa na Arsenal uwanjani Emirates katika mchezo wa ligi kuu Uingereza. Na hichi ndicho alichokisema;-

Alipoulizwa juu ya tetesi za Chiellini kutakiwa na Chelsea
Conte alijibu "Umesema vizuri, i tetesi na kuna tetesi ambazo huwa za kweli na nyengine zinabaki kuwa tetesi. Kipindi hiki cha usajili, klabu huwa zipo kwenye wakati mgumu kutokana na hizo tetesi, ila muhimu Chiellini ni mchezaji bora lakini nadhani anataka kumaliza maisha yake ya soka klabuni Juventus"

Alipoulizwa juu ya usajili
Conte alijibu "Majukumu yangu ni kuiweka timu iwe sawa na kuuambia uongozi nahitaji mchezaji wa nafasi gani ili iweze kuchagua chaguo bora zaidi kwa nafasi hiyo na waweze kumsajili. Mi majukumu yangu ni kuifanya timu iwe uwanjani na kama kocha natakiwa kuifanya timu iwe bora uwanjani"

"Hatuna kikosi kipana kinachoweza kutufanya tuweze kuuza ama kumtoa mchezaji kwa mkopo, nadhani hilo ndio kubwa lakini pia mpaka ukiona mchezaji anauzwa basi jua kuna mbadala wake amefika" alijibu Conte.

Alipoulizwa kuhusu fedha za Diego Costa
Conte alijibu "Sio jukumu langu kuongelea hilo, ni majukumu ya timu"

Kuhusu kuwarudisha makinda walioko kwa mkopo
Conte alijibu "Sina uhakika katika hilo ukizingatia tuliowatoa kwa mkopo wanapata nafasi ya kucheza huko walipo. Mwezi januari mwaka 2017 tuliwarudishwa Nathan Ake, Kenedy na Musonda lakini kwa msimu huu sina uhakika"

Kuhusu maendeleo ya David Luiz
Conte alijibu "anaendelea vizuri, na huenda akacheza kwenye mchezo dhidi ya Norwich, amefanya mazoezi na timu kwa siku mbili. Wakati huohuo kuna jambo nalielewa kuwa mchezaji asipoweza kucheza kama kawaida wakati ameshazoea kucheza mara kwa mara huwa kuna kutoeleweka kama huku ila nataka kusema ninajivunia kufanya kazi na kuwa na mchezaji kama huyu"

Kuhusu majeruhi
Conte alijibu "Ni Musonda pamoja na Luiz tu, ndio hawatokuwepo kwenye mchezo huu ila nategemea kuwa nao kwenye mchezo dhidi ya Norwich na kwa wengine wote wapo sawa na nitakuwa nao kama kawaida"

Kuhusu kucheza dhidi ya Arsenal
Conte alijibu "Mara zote huwa ni mchezo mgumu kucheza dhidi yao ila muhimu ni kufanya vizuri kwa ajili ya mashabiki na hata kujiweka pazuri kwenye msimamo wa ligi kuu.

Kuhusu kubadilisha wachezaji
Conte alijibu "Kwa timu yangu ni muhimu kutuia wachezaji wote na kufanya mabadiliko zaidi kwenye kikosi ila nachoshukuru katika hilo nafanya mabadiliko na bado tunapata matokeo mazuri, najivunia kwa hilo. Inaonyesha wachezaji wanafanya vizuri"

***Hayo ni baadhi ya aliyoyaongea kocha huyo kuelkea mchezo huo lakini sisi kama mashabiki wa Chelsea tumefurahishwa kumskikia kocha akikiri hana tatizo na David Luiz maana ni kipenzi chakaribu kila  mchezaji na shabiki wa Chelsea, na kuna wasiwasi huenda kuondoka kwake kama ikitokea kutatoa ushirikiano na kutengeneza makundi kwa klabu na kufanya timu kufanya vibaya haswa pale mchezaji anapoondoka kwa hali mbaya bila maelewano mazuroi.

No comments:

Post a Comment