MKONGWE WA CHELSEA AMSHANGAA MORATA - Darajani 1905

MKONGWE WA CHELSEA AMSHANGAA MORATA

Share This
Mkongwe wa klabu ya Chelsea, Tony Cascarino
aliyewai kucheza Chelsea kuanzia mwaka 1992 mpaka mwaka 1994 amemjia juu mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata juu ya mtindo wake wa kufunga zaidi kwa kichwa kuliko kutumia miguu.

"Kuna wachezaji wengi wapo vizuri kichwani kulikomm miguuni katika ufungaji, kama alivyo Andy Caroll. Sasa natambua ata Morata aliyeigharimu Chelsea kisi cha paundi milioni 60 katika kumsajili naye ni mmojawao" alisema mkongwe hyuyo ambaye kwa sasa anafanya kazi kama mchambuzi wa soka na mwandishi wa habari.

"Kama ukimpatia mipira tisa kati ya kumi kichwani basi atafunga, ila kwa miguu ameshakosa nafasi nyingi rahisi za kufunga. Unafikiri ni rahisi zaidi kufunga kwa miguu lakini yeye anakosa" alisema mchambuzi huyo ambaye aliichezea Chelsea michezo 40 na kufunga magoli 8.

Alvaro Morata aliwai kuulizwa kwanini ana uwezo mkubwa wa kufunga kwa kichwa alisema anadhani kutokana na pindi alipokuwa mdogo baba yake kumfundisha zaidi kutumia kichwa na alikuwa napenda zaidi kupiga mpira kwa kichwa kutokana na kujisikia vizuri pindi anaporuka juu

Morata mpaka sasa ameshaichezea Chelseajumla ya michezo 27 na kuifungia magoli 13 huku kwenye ligi kuu akicheza michezo 18 akifunga magoli 10 huku akitumia kichwa kufunga magoli 6 na manne akifunga kwa miguu.

No comments:

Post a Comment