Kuelekea mchezo wa ligi kuu kati ya Chelsea ikikaribishwa na Arsenal hapo kesho uwanjani, Emirates huenda kocha wa Arsenyani (Arsenal), Arsene Wenger akapokea adhabu kuelekea kwenye mchezo huo ambao Chelsea itahitaji alama tatu ili irudi kwenye nafasi ya pili iliyokuwa mwanzo kabla ya kushushwa na Manyumbu (Man utd) baada ya kushinda jana.
Chama cha soka Uingereza maarufu kama FA huenda kikamuadhibu kocha Wenger kutokana na tukio alilolifanya katikamchezo wa ligi kuu alipoonekana akibishana na maamuzi ya mwamuzi Mike Dean alipoamuru West Brom wapige penati kutokana na mlinzi wa klabu ya Arsenyani, Calum Chambes kushika katika eneo la hatari ambapo maamuzi hayo yalitokea dakika za amajeruhi za mchezo huo na kuifanyana Arsenyani ishindwe kupata ushindi na kuishia kusuluhu kwa sare ya 1-1.
Msemaji wa FA amesema kunafanyika uchunguzi wa nini alichokitamka kocha Arsene Wenger na hata kama kuna tukio lilitendwa kinyum na kocha huyo basi adhabu itamkumba.
Chelsea itashuka katika mchezo huo ikiendelea kuwakosa David Luiz na Charly Musonda ambao wao wanatarajiwa kurudi uwanjani katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya Norwich city, jumamosi hii.
Wakati kwa upande wa Arsenyani inatajwa kuwakosa nyota wake kama Monreal, Konscielny, Ozil, Ramsey pamoja na Giroud ambao wanauguza majeraha.
WENGER KUIKOSA CHELSEA?
Share This
Tags
# Chelsea Habari
# Majirani
Share This
About Darajani 1905
Majirani
Labels:
Chelsea Habari,
Majirani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment