Nyota wa zamani wa klabu ya Chelsea, John Obi Mikel amekutwa na majanga katika kipindi iki akiwa ametoka kuiongoza timu yake ya taifa ya Nigeria kwenye michuano ya Kombe la Dunia huko nchini Urusi.
Tarehe 29-Juni mwaka huu kuliripotiwa taarifa kwamba baba mzazi wa nyota huyo anayeitwa Obi Michael alitekwa na watu wasiojulikana akiwa njiani akirejea nyumbani akiwa pamoja na dereva wake. Wakiwa njiani huko nchini Nigeria kwenye gari la Toyota lenye namba MUS 604CG walivamiwa na wavamizi wenye silaha na kuwaweka mafichoni kwenye moja ya misitu nchini humo.
Hii leo mkuu wa polisi wa Wilaya ya Enugu ya huko nchini ametoa taarifa akisema jeshi la polisi nchini humo limefanikiwa kumuokoa mzee huyo akiwa salama lakini walipata upinzani mkubwa wakirushiana risasi na majambazi hao. Lakini kutokana na umahiri wa polisi walifanikiwa kuwashinda na kufanikiwa kumuokoa mzee huyo akiwa pamoja na dereva wake.
Watekaji hao walidai kutaka kiasi cha fedha cha Naira milioni 10 ili kumuachia baba mzazi wa nyota huyo ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya nchini China.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment