Chelsea inamsaka mlinda mlango atakayeziba pengo la mlinda mlango wa sasa, Thibaut Courtois anayehofiwa kuweza kujiunga na klabu ya Real Madrid ambayo inamsaka kipa atakayekuwa chaguo la kwanza klabuni hapo.
Makipa wengi wanatajwa kufukuziwa na klabu hiyo wakiwemo Gianluigi Donarumma, Alisson Becker na mlinda mlango wa Kasper Schmeichel. Lakini sasa jina la mlinda mlango nambari mbili wa Barcelona, Jasper Cillessen.
Jasper Cillessen mwenye miaka 29 anatajwa anafukuziwa na Chelsea huku dau lake ambalo inatakiwa klabu ilipe ili imsajili likiwa ni paundi milioni 60 lakini inadhaniwa kwamba klabu yake ya Barcelona itakuwa tayari kupokea paundi milioni 30 ambayo ni nusu ya dau lililokuwepo kwenye mkataba wake.
No comments:
Post a Comment