Unajua sababu ya kuchelewa kwa usajili Sarri kutua Chelsea? - Darajani 1905

Unajua sababu ya kuchelewa kwa usajili Sarri kutua Chelsea?

Share This

Wiki iliyopita nilikuletea taarifa kwamba chanzo cha kuaminika kimeripoti kwamba klabu ya Chelsea inaweza kukamilisha usajili wa kocha Maurizio Sarri kutoka klabu ya nchini Napoli, Maurizzio Sarri.

Lakini usajili huo haujakamilika mpaka sasa, je sababu ni nini?

Kuna taarifa mpya ambazo zimedai kuchelewa kukamilika kwa kocha huyo mwenye miaka 59 kutua Chelsea ni kutokana na kiongozi mkubwa wa klabu ya Napoli kumkatalia kocha huyo kuondoka na nyota watatu wa klabu hiyo.

Nyota hao ambao ni Kalidou Koulibaly, Elseid Hysaj na Piotr Zielinski wanatajwa kutakiwa na kocha huyo pindi atakapokamilisha usajili wake wa kujiunga na Chelsea lakini kiongozi huyo hayupo tayari kuona jambo hilo linatokea na hivyo kuamua kukazia usajili huo usikamilike.

Sarri anatajwa kuwa na thamani ya euro milioni 8 anatajwa kufikia makubaliano na Chelsea ili kujiunga na klabu hiyo lakini Napoli ambayo imeshamnasa kocha huyo inakataa kumtoa kisa kutotaka kuwapoteza nyota wake.

Kuoata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment