Hatimaye kile nilichokisema kimetimia, Eden Hazard uso kwa uso na Willian kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea huko nchini Urusi.
Mchezo wa mapema ulikuwa wa Brazil ikicheza dhidi ya Mexico ambapo mchezo ulichezwa na hatimaye Willian Borges akaiwezesha timu yake ya Brazil kupata ushindi wa magoli 2-0 huku mwenyewe akichangia kufungwa kwa goli la kwanza akitokea pasi ya mwisho.
Mara baada ya mchezo huo kuchezwa mishale ya saa 17:00 kwa saa za Afrika Mashariki hatimaye muda ukasogea na ikawa zamu ya nyota wengine wa Chelsea ambapo nahodha wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Eden Hazard aliungana na nyota wengine wa Chelsea, Thibaut Courtois pamoja na Michy Batshuayi kucheza mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya Japan.
Ubelgiji akafanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-2 huku nyota wa Chelsea, Eden Hazard ambaye alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo huo pamoja na Thibaut Courtois wakicheza kwa dakika zote za mchezo wakati kwa upande wa Michy Batshuayi akisalia kwenye benchi.
Kwa matokeo hayo yanamaanisha sasa Ubelgiji itacheza dhidi ya Brazil katika hatua ya robo fainali.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment