Chelsea yavutiwa na nyota wa Denmark, yaanza kumfukuzia - Darajani 1905

Chelsea yavutiwa na nyota wa Denmark, yaanza kumfukuzia

Share This

Alionyesha uwezo mkubwa usiku wa jana pindi alipoiongoza timu yake ya taifa ya Denmark katika mchezo wa Kombe la Dunia ambapo walimenyana dhidi ya Croatia akiokoa penati ya Luca Modric kwa dakika za majeruhi za muda wa nyongeza na kufanya mchezo huo uliomalizika kwa sare ya 1-1 kwenda kwenye hatua ya kupigiana mikwaju ya penati ambapo huko nako aliokoa penati mbili ila bahati haikuwa kwao wakafungwa 3-2 na kuondoshwa kwenye michuano hiyo.

Ni Kasper Schemeichel ambaye ni mtoto wa mlinda mlango wa zamani anatajwa kuziingiza klabu za Chelsea na As Roma kumgombania.

Kipa huyo anayeichezea klabu ya Leicester city ya nchini Uingereza anatajwa kuitamanisha Chelsea ambayo inawasiwasi wa kuachana na mlinda mlango wake nambari moja, Thibaut Courtois. Lakini pia klabu ya As Roma inamtaka mlinda mlango huyo mwenye miaka 31 kama sehemu ya kumfukuzia mrithi wa mlinda mlango wake wa sasa, Alisson Becker ambaye anatajwa kufukuziwa.

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment