Rasmi; Nyota wa Chelsea atimkia Uholanzi - Darajani 1905

Rasmi; Nyota wa Chelsea atimkia Uholanzi

Share This

Alianza maisha yake ya soka kwenye akademi ya Chelsea kabla ya baadae kupelekwa Sutton United kabla ya baadae kurejea tena Chelsea akiwa kwenye akademi lakini baadae akapandishwa kwenye kikosi cha wakubwa ambapo huko hakufanikiwa kupata nafasi ya kuichezea klabu hiyo.

Hatimaye akapelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya Bristol na msimu uliopita aliutumia akiwa kwa mkopo kwenye klabu ya Sunderland.

Hatimaye sasa nyota wa kikosi cha Chelsea mwenye miaka 20, Jake-Lehim Clarke-Salter ambaye siku kadhaa alikuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa la Uingereza chini ya miaka 21 kilichoshinda taji amekamilisha usajili wake wa mkopo wa muda mrefu.

Clarke-Salter amekamilisha uhamisho wa kujiunga na klabu ya Vitesse ya nchini Uholanzi. Vitesse imemsajili nyota huyo na inaendelea kudumisha mahusiano mazuri na klabu ya Chelsea maana imeshawachukua nyota wengi kutoka klabuni hapo ikiwanoa kwa kuwatumia kwa mkopo.

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment