HAZARD MCHEZAJI BORA UBELGIJI, UKU CHELSEA IKITAWALA - Darajani 1905

HAZARD MCHEZAJI BORA UBELGIJI, UKU CHELSEA IKITAWALA

Share This
Winga na mshambuliaji wa Chelsea, Eden Hazard amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ubelgiji kwa mwaka 2017.

Eden Hazard ameshinda tunzo hiyo akiwapiku nyota kadhaa huku Kevin De Bruyne akishika nafasi ya pili kati ya washindi watatu.
Hazard ameshinda tunzo hiyo akipigiwa kura jumla 10,280 huku De Bruyne aliyewai kuichezea Chelsea ambaye kwa sasa anaichezea Mama site(Man city) akipata kura 4,710 na nafasi ya tatu ikishikwa na Romelu Lukaku ambaye nae alianza maisha ya soka la Uingereza akiwa Chelsea akisajiliwa kutoka Anderlecht ambaye kwa sasa akiichezea Manyumbu(Man utd) akipata kura 3,223.

Hongera kwa Eden Hazard.

No comments:

Post a Comment