Chelsea leo inashuka uwanjani ikikaribishwa na Arsenal kucheza mchezo wa ligi kuu Uingereza ambapo Chelsea itakuwa ugenini katika uwanja wa Emirates.
Lakini wakati Chelsea ikishuka katika mchezo huo, ile kiu ya mashabiki wengi wa Chelsea wakitaka kujua kuna tatizo gani kati ya kocha Antonio Conte na mlinzi wa Chelsea, David Luiz na kama kuna tofauti baina ya watu hao basi kila shabiki alitamani kuona tofauti hizo zikizikwa maana hawakupenda kumuona kipenzi chao David Luiz akiachana na klabu hiyo aliyojiunga nayo kwa mara pili msimu wa 2016-2017 na kuisaidia kutwaa taji la ligi kuu.
Kocha Antonio Conte alipohojiwa juu ya matumaini ya nyota huyo kuhusu kurejea kwake uwanjani Conte alijibu "anaendelea vizuri, na huenda akacheza kwenye mchezo dhidi ya Norwich, amefanya mazoezi na timu kwa siku mbili. Wakati huohuo kuna jambo nalielewa kuwa mchezaji asipoweza kucheza kama kawaida wakati ameshazoea kucheza mara kwa mara huwa kuna kutoeleweka kama huku ila nataka kusema ninajivunia kufanya kazi na kuwa na mchezaji kama huyu"
Ambapo kauli hiyo inaonyesha kuwa kocha huyo hana kinyongo na raia huyo mbrazili na ni kinyume na taarifa zilizokuwa zikienea mwanzo kuwa chuki ya kocha huyo kwa mchezaji huyo ndiyo inamfanya kocha Conte amweke nje na nafasi yake kuchukuliwa na Andreas Christensen.
David Luiz aliichezea Chelsea mchezo wake wa mwisho mwezi Oktoba mwaka jana mara baada ya Chelsea kukubali kichapo cha mabao 3-0 na hivyo kuenezwa taarifa kuwa Conte amekorofishana na David Luiz mara baada ya kucheza chini ya kiwango katika mchezo huo.
No comments:
Post a Comment