HABARI MUHIMU KUELEKEA ARSENAL vs CHELSEA - Darajani 1905

HABARI MUHIMU KUELEKEA ARSENAL vs CHELSEA

Share This
Chelsea leo itashuka uwanja wa Emirates uliochini ya klabu ya Arsenal kucheza mchezo wa ligi kuu kwa raundi ya 22 ambapo Chelsea inahitaji alama tatu ili ijiweke sawa katika mbio zake za kugombania ubingwa.
Hapa nimekuletea mambo muhimu unayopaswa kuyajua kuelekea mchezo huo.
Mwamuzi; Anthony Taylor, aliwai kuchezesha mechi kadhaa za Chelsea, ambapo alikuwa mwamuzi katika mchezo ambao Chelsea ilimenyana na Tottenham katika mchezo uliopigwa White Hart Lane na Chelsea ilishinda 2-1 huku pia akiwa mwamuzi katika mchezo ambao Chelsea iliibamiza Manyumbu(Man utd) kwa goli 1-0.
Chelsea Majeruhi; Chelsea itashuka kwenye mchezo huu ikiendelea kuwakosa nyota wake David Luiz na Charly Musonda ambao wanategemewa kurudi kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Norwich.
Arsenal Majeruhi; Arsenal inaelezwa kuwakosa nyota wake kadhaa akiwemo Mesut Ozil, Kolasinac, Aaron Ramsey, Monreal na Olivier Giroud
H2H; Mara ya mwisho, Chelsea kupata ushindi katika uwanja huu ilikuwa mwaka 2012 katika kombe la ligi, Chelsea ikishinda 2-1 magoli yakifungwa na Fernando Torres pamoja na Juan Mata.
Mechi zilizopita;
Chelsea, WWDWW
Arsenal, WWDWD
Muda; Saa 10:45 usiku kwa saa za Afrika Mashariki (saa 22:45)

No comments:

Post a Comment