CONTE TAYARI KUWAUZA LUIZ NA MICHY - Darajani 1905

CONTE TAYARI KUWAUZA LUIZ NA MICHY

Share This

Kumekuwa na mwendelezo wa tetesi na fununu zikiwahusu nyota wa Chelsea kutaka kuondoka klabuni. Tetesi hizo zimemfanya kocha wa Chelsea, Antonio Conte kuwajibu nyota hao ambao wanatajwa kuondoka.

Kumekuwa na taarifa zikimhusisha David Luiz ambaye anaonekana kupoteza nafasi katika kikosi cha kwanza akicheza mchezo wake wa mwisho mwezi Oktoba mwaka 2017 dhidi ya As Roma kuhusishwa kutaka kuondoka klabuni hapo huku Michy Batshuayi nae akielezwa kutaka kuondoka mara baada ya kuona nafasi yake kikosini ni finyu.

Kocha Conte amesema "Naelewa maana ata mi nilikuwa mchezaji, katika kipindi iki kuelekea kombe la dunia kila mchezaji anataka kucheza zaidi ili aweze kuchaguliwa timu ya taifa. Lakini nachotaka kusema kama kuna mchezaji akiona hana furaha ya kuendelea kubaki klabuni, basi sitaki kuwa kikwazo kwake, anaweza kuondoka"

"Lakini kikubwa siwezi kumtoa mchezaji kwa mkopo au kumuuza bila kuleta wa kuziba pengo lake"

"Kama kuna mchezaji yoyote ataona hana furaha klabuni anaweza kuondoka maana nataka kuwa na mchezaji mwenye furaha kuwa hapa sio yupo hapa lakini hana furaha, atatuambukiza hiyo ata sisi na hata watu wengine kwenye timu" alisema Conte.

No comments:

Post a Comment