HAZARD KUTIMKIA MADRID - Darajani 1905

HAZARD KUTIMKIA MADRID

Share This
Mwandishi wa habari za michezo na mchambuzi wa michezo katika chombo cha ESPN, Sid Lowe anaamini Hazard anaweza akaungana na Real Madrid muda wowote katika dirisha hili dogo la usajili uku akiwa na mkataba klabuni Chelsea unaoisha mwaka 2019.

"Naamini anaweza akaachana na Chelsea muda wowote kutokana na maneno alioyoongea baba yake" alisema Lowe.

"Ni ngumu kumtoa Hazard pale Chelsea, lakini maneno ya baba yake yanaweza kuchochea kasi ya nyota huyo kuweza kufukuziwa zaidi na Madrid ili imsajili. Hakuna ubishi kwa maneno aliyoongea baba yake hadharani yanaweza kumfanya mchezaji huyo aungane na Chelsea haraka sana" aliongezea mchambuzi huyo.

Baba yake na Hazard anayeitwa Thierry Hazard alihojiwa na chombo kimoja cha habari juu ya hatma ya nyota huyo klabuni Chelsea na alichokisema kwamba mchezaji huyo amesitisha kusaini mkataba mpya wa kuzidi kuendelea kuwa Chelsea ili aangalie kama Real Madrid wanaweza kumsajili haraka au itakuwaje, ambapo maneno hayo yanamfanya mchambuzi huyo aamini kuna uwezekano mkubwa wa nyota huyo kuondoka Chelsea.

***Kama mashabiki tumechoshwa na kinachoendelea kwa Hazard kikubwa afanye chaguo sahihi kama anaona ana maisha zaidi klabuni Chelsea basi asaini mkataba mpya na kama anaona hana furaha kuendelea kubaki basi atuachie timu yetu.

No comments:

Post a Comment