WENGER vs CONTE KUELEKEA LEO USIKU - Darajani 1905

WENGER vs CONTE KUELEKEA LEO USIKU

Share This
Kuelekea mchezo wa leo usiku kati ya Chelsea dhidi ya Arsenyani(Arsenal) leo usiku huku Chelsea ikiwa ugenini, hapa nimekuletea maneno ya makocha wa timu hizo, yaani Arsene Wenger akiwa kama kocha wa Arsenyani na Antonio Conte akiwa kama kocha wa Chelsea kuelekea mchezo huo utakaochezwa saa 10:45 usiku (saa 22:45) kwa saa za Afrika Mashariki.

Alichokisema Antonio Conte "Mara zote huwa ni mchezo mgumu kucheza dhidi yao ila muhimu ni kufanya vizuri kwa ajili ya mashabiki na hata kujiweka pazuri kwenye msimamo wa ligi kuu"

Alichokisema Arsene Wenger "Chelsea imerudi katika hali nzuri kwa sasa, na wamekuwana matokeo mazuri. Nadhani utakuwa mchezo mgumu"

Chelsea inahitaji ushindi usiku wa leo ili ijiweke sawa katika msimamo wa ligi kuu Uingereza, ambapo kama ikishinda leo itafanikiwa kupanda kutoka nafasi ya tatu iliyopo sasa mpaka nafasi ya pili ambapo itafikisha alama 48, huku kwa upande wa Arsenyani wao kama ikitokea wakishinda watapanda kutoka nafasi ya sita iliyoko hivi sasa mpaka nafasi ya tano ambayo inashikwa na Tottenham.

No comments:

Post a Comment