Kocha wa Chelsea, Antonio Conte anatajwa kwa karibu kumfukuzia nyota wa Everton, Ross Barkley huku akipata upinzani kutoka kwa Tottenham ambayo nayo inatajwa kumuwania kiungo huyo.
Chelsea inapewa nafasi kubwa kumnasa Barkley kutokana na kutaka kupeleka maombi katika dirisha hili dogo la usajili kwa klabu ya Everton wakati Tottenham imepanga kumnasa nyota huyo katika dirisha kubwa la usajili litakalokuwa mwishoni mwa msimu.
Barkley ilikuwa atue klabuni Chelsea toka katika dirisha kubwa la usajili ambapo mchezaji huyo aligoma ghafla akiwa kwenye vipimo akisema alitaka kuhama Everton mpaka pale atakapopona maradhi yake yaliyomfanya kukaa nje, ingawa sasa kuna taarifa kuwa majeraha hayo yashapona na ashaanza mazoezi klabuni Everton.
No comments:
Post a Comment