Klabu ya Barcelona inatajwa kuingia sokoni kumsaka mlinzi wa kati mwenye uwezo wa kumiliki na kucheza mpira ambapo kunatajwa kuwepo wa wasiwasi wa kwenda Chelsea na kumtaka mlinzi Andreas Christensen.
Christensen amekuwa na uwiano mzuri katika kumiliki mpira na kutoa pasi za uhakika na kunatajwa huenda Barcelona ikamuwania katika dirisha hili la usajili ambapo klabu ya Barcelona inatajwa kumhitaji mlinzi wa aina ya Christensen.
Barcelona inatajwa kumuuza mlinzi wake Javier Mascherano katika dirisha la usajili la mwezi januari na huenda ikamhitaji wa kuziba nafasi yake.
No comments:
Post a Comment