WACHINA KUIPIGA CHINI CHELSEA - Darajani 1905

WACHINA KUIPIGA CHINI CHELSEA

Share This

Mwaka 2017 ndio unaisha na sasa mwaka 2018 unakaribia kuingia ambapo wakati mwaka huo ukiingia klabu nazo zitafanya usajili katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari. Klabu ya Chelsea katika moja ya nyota inayotajwa kumfukuzia ni nyota raia wa Brazil, Lucas Moura mwenye miaka 25 anayetajwa kutokuwa na chake tena klabuni PSG ambapo anaonekana hana nafasi.

Chelsea ni moja kati ya klabu zilizokuwa zinapewa nafasi kumsajili nyota huyo ambaye mwenye hataki kucheza nje ya bara la Ulaya, lakini sasa klabu kutoka nchini China kwenye bara la Asia, Herbei Fortune inatajwa kupeleka maombi ya kumsajili nyota huyo ambapo inaelezwa kuna uwezekano wakatoa dau kubwa litakaloishawishi klabu yake ya PSG kumuuza kwenda klabuni hapo.

Klabu ya Manyumbu (Man utd) nayo inatajwa kumuwania nyota huyo.

No comments:

Post a Comment