WILLIAN AWA NYOTA WA SIKU - Darajani 1905

WILLIAN AWA NYOTA WA SIKU

Share This

Mara baada ya kuiongoza Chelsea kuibamiza Stoke city kwa magoli 5-0 huku Willian akitengeneza nafasi nyingi zaidi ambapo ametengeneza magoli mawili yaliyofungwa na Antonio Rudiger pamoja na Pedro Rodriguez huku mwenyewe akifunga goli moja, Willian amechaguliwa kuwa nyota wa mchezo huo dhidi ya Stoke city.

Mara baada ya kuchaguliwa kwake, nasi kama Darajani 1905 tumemchagua nyota huyo kuwa nyota wa siku na hata nyota wa mwaka mpya maana kwa ubora wake ameifanya Chelsea ipande kutoka nafasi ya tatu mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu na ivuke kuingia mwaka 2017 ikiwa nafasi ya pili.

Kwa maana hiyo maana ya kuwa nyota wa siku maana yake katika wiki yote hii nitakuwa nakuletea matukio aliyoyafanya nyota huyo klabuni Chelsea na maisha yake binafsi mpaka mwisho itakuwa pale Chelsea itakaposhuka uwanjani kumenyana na Arsenal katika mchezo mwengine wa ligi kuu tarehe 03-Januari.

No comments:

Post a Comment