Mwaka 2017 unaelekea kuisha, tukiwa tumebakiza masaa kadhaa ili kuumaliza mwaka huo.
Na katika mwaka wote huo, Chelsea imepitia katika vipindi tofauti tofauti kama kupata mambo ya huzuni na hata furaha pia, na kama mchezoni kushuhudia tukipoteza michezo muhimu na hata kupata ushindi katika michezo iliyotuacha tukiwa na furaha.
Lakini kwa upande wa kocha Antonio Conte, mwaka 2017 ni moja kati ya vitu havitokuja kupotea akilini mwake. Kumekuwa na matukio mengi kwa upande wake lakini jambo kubwa lililomfanya abaki akiamini mwaka 2017 ndio mwaka bora kwake ni pale alipoisaidia Chelsea kutwaa taji la ligi kuu Uingereza tena akifanya hivyo ukiwa ni msimu wake wa kwanza katika ligi kuu Uingereza. Lakini pia akitimiza idadi chache ya makocha raia wa Italia kuwai kutwaa taji la ligi kuu.
Carlo Ancelloti, Claudio Ranieri, Roberto Mancini ni baadhi ya makocha waliowai kutwaa taji hilo klabuni huku sasa Conte nae akiwa mmojawapo.
"Ulikuwa ni mwaka bora kwangu, nadhani itakuwa ni ngumu sana kuusahau akilini" alisema Antonio Conte.
Chelsea inatimiza alama 45 na kupanda kutoka nafasi ya tatu mpaka nafasi ya pili ikiishusha klabu ya Manyumbu(Man utd) ambapo kwa alama izo inamaana zimebaki alama 13 kuifikia Mama Site(Man city) iliyoko nafasi ya kwanza kileleni.
No comments:
Post a Comment