DIEGO COSTA RASMI ATLETICO MADRID - Darajani 1905

DIEGO COSTA RASMI ATLETICO MADRID

Share This

Aliyekuwa mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa ametambulishwa rasmi katika klabu yake mpya ya Atletico Madrid aliyojiunga toka dirisha kubwa la usajili.

Diego Costa aliyeondoka Chelsea kutokana na kuwa na mgogoro mkubwa na kocha Antonio Conte aliungana na Atletico Madrid toka mwezi Agosti kwenye dirisha kubwa la usajili ingawa hakuruhusiwa kucheza mchezo wowote wa kiushindani kutokana na klabu ya Atletico Madrid ilikuwa kwenye kifungo cha kutoruhusiwa kufanya usajili.

Diego Costa amepewa namba 18 kwenye klabu hiyo yenye makazi yake kwenye jiji la Madrid.

No comments:

Post a Comment