REAL MADRID WAIPA CHELSEA DAU LA DUNIA KWA HAZARD - Darajani 1905

REAL MADRID WAIPA CHELSEA DAU LA DUNIA KWA HAZARD

Share This
Klabu ya Real Madrid inatajwa kupeleka ofa zakimafia kwa klabu ya Chelsea ili kumsajili nyota wake raia wa Ubelgiji, Eden Hazard.
Gazeti la The Sun limeripoti kuwa Real Madrid imeandaa donge nono ili kumnasa nyota huyo ambaye amefanywa na kocha Zinedine Zidane kuwa chaguo la kwanza.

Real Madrid inatajwa ipo tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 120 ili kumnasa nyota huyo ambaye mchezo wa jana ambapo Chelsea ilimenyana na Stoke city hakupewa nafasi kabisa ya kucheza mchezo huo huku kocha Antonio Conte akidai kumweka kwake nje ni kutaka kumfanya nyota huyo apumzike ili awe sawa katika michezo ijayo.

Kwa dau hilo la paundi milioni 120 litamfanya Hazard kuwa mchezaji ghali kusajiliwa kutokea ligi kuu Uingereza.

No comments:

Post a Comment