COSTA; NAJIVUNIA KUWA CHELSEA - Darajani 1905

COSTA; NAJIVUNIA KUWA CHELSEA

Share This

Mshambuliaji mpya wa Atletico Madrid aliyesajiliwa akitokea Chelsea, Diego Costa ametambulishwa leo rasmi klabuni Atletico mara baada ya kujiunga na klabu hiyo toka mwezi Agosti ambapo alikuwa kwenye mgogoro na kocha wa Chelsea, Antonio Conte.

Mara baada ya kutambulishwa leo, Diego Costa alisema "Nafurahi kutimiza ndoto zangu za muda mrefu za kurudi Atletico maana leo zimetimia, ni kweli hatujafanikiwa kufuzu kwenye klabu bingwa ila nitapambana kuhakikisha klabu inapata kile inachostahili. Wakati nikiwa nje nilikuwa natamani kurudi uwanjani ili kuisadia timu. Naiheshimu Chelsea na nimejifunza mengi kutokea kule na nimekuwa na historia nzuri klabuni pale"

Diego Costa alijiunga rasmi na Chelsea mwaka 2014 akitokea Atletico kwa dau la paundi milioni 32 huku akiisaidia Chelsea kutwaa taji la ligi kuu Uingereza mara mbili na kombe la ligi.

No comments:

Post a Comment