Mara baada ya kutokuwa na maelewano mazuri pindi Diego Costa alipokuwa klabuni Chelsea chini ya kocha Antonio Conte na leo nyota huyo kutambulishwa kuwa mchezaji rasmi wa Atletico Madrid.
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte ametoa neno kumuaga nyota huyo raia wa Hispania, Conte amesema "huwa sipendi kumuongelea mchezaji wa timu nyengine, naliheshimu hilo ila nafurahi kufanya kazi na mtu tuliyepambana pamoja mpaka kufikia mafanikio, nakumbuka mengi kutoka kwake"
Diego Costa aligoma kuondoka Chelsea mara baada ya kuwa na mawasiliano mabaya na kocha huyo akimtuhumu kumtumia ujumbe wa simu akimwambia hatokuwa kwenye mipango yake katika msimu ujao mara baada ya kuisaidia Chelsea kutwaa taji la ligi kuu.
Je unamkumbuka kwa jambo gani Diego Costa? unadhani Chelsea itakuwa bora kwa kukosekana kwake?
No comments:
Post a Comment