KARIBU MWAKA 2018 - Darajani 1905

Ni wiki moja na siku tano zimepita toka kuanzisha kwa ukurasa huu wa Darajani 1905 na leo tunaenda kushukuru pamoja kwa kuingia mwaka 2018 na kuuacha mwaka 2017 ambao kwa mashabiki na wapenzi wa soka utabaki katika vichwa vya wengi kutokana na matukio mengi ya furaha na ya uzuni pia lakini bila kusahau kuwatakia pole wale walioguswa kwa namna moja ama nyengine katika lile tukio la ajali ya ndege la nchini Brazil lililowaacha wengi wakiuzunika na kulia huku wachezaji kadhaa tu wakinusurika.

Lakini mwaka 2017 utabaki kuwa wa historia pia kwa mashabiki wa Chelsea kutokana na mambo mengi matamu yaliyotokea ndani yake lakini kubwa ni ubingwa wa ligi kuu Uingereza, ikibeba chini ya kocha Antonio Conte.

Nasema asante pia kwa kila mmoja aliyehusika kwa namna moja ama nyengine katika ukurasa wetu huu wa Darajani 1905. Nasema asante kwa wote maana bila nyinyi ukurasa huu usingefikia hapa ulipofikia.

Asanteni sanaaa na heri ya mwaka mpya kwenu

No comments:

Post a Comment