ASANTE MUNGU KWA MWAKA 2018 - Darajani 1905

Sasa ni rasmi tumeingia mwaka 2018, kila mtu ana furaha kuufikia mwaka huu ambao kila mtu ana ndoto na mipango mingi ya kuweza kufanya mwaka huu ili aweze kujiweka sawa kimaisha.

Najua mitandao mingi inatumiwa na vijana, hata ukurasa huu unatembelewa na watu wengi lakini bila shaka vijana ndio wengi katika familia hii ya Darajani 1905. Muhimu ni kuwa na mipango na ndoto ambazo unaona unaishi katika ndoto hiyo na uone majaribu kwako ni kama manukato, na kukosolewa ni kama changamoto. Usiogope kupambana na usikate tamaa, kama mimi mwandishi wako navyojitahidi kupambana ingawa kuna kipindi unapatwa na vikwazo ambavyo vinakaribia kunidondosha na kunifanya nijihisi kushindwa katika ndoto yangu au ndoto zangu.

Lakini Mungu ndio pekee wakunifanya nirudi kwenye mstari na niamini pale ambapo ni ngumu mtu mwengine kupaamini.

Nami kwakuwa ni kijana kama vijana wengi wanaotembelea ukurasa huu natoa fursa kama kuna mtu awe kijana wa jinsia yoyote au ata mtu mzima wa jinsia yoyote kama anadhani tunaweza kushirikiana kwa namna moja ama nyengine, lakini pia unaweza kutangaza kupitia ukurasa huu.
Mawasiliano
Simu namba; +255629964908
E-mail; eng.bakayoko@gmail.com

No comments:

Post a Comment