WILLIAN; NINA FURAHA CHELSEA - Darajani 1905

WILLIAN; NINA FURAHA CHELSEA

Share This

Kiungo na winga wa Chelsea, Willian da Silva Borges amewajibu wale wanaomfikiria kuondoka klabuni hapo.

Willian alipohojiwa kuhusu fununu hizo alisema "kumekuwa na tetesi za kutakiwa na Palmeiras lakini sihitaji kuondoka Chelsea, nahitaji watu waelewe, nina furaha ya kuwa Chelsea"

Willian amekuwa hana uhakika wa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza ambapo nafasi ya washambuliaji wawili mbele inawafanya Eden Hazard na Alvaro Morata kupata nafasi zaidi katika mfumo wa 3-5-2 ambao umekuwa ukitumiwa sana na kocha Antonio Conte msimu huu.

Willian alifanya vizuri katika mchezo wa juzi dhidi ya Stoke city huku akihusika zaidi katika magoli ya Chelsea iliyotoka kimasomaso kwa magoli 5-0 huku Willian akifunga kwa mkwaju wa penati. Willian alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment