CONTE KUWALETA SERENGETI BOYS - Darajani 1905

CONTE KUWALETA SERENGETI BOYS

Share This

Mara baada ya kuondokewa na wakongwe walioacha alama kubwa klabuni Chelsea ambao ni kama John Obi Mikel aliyetimkia China, John Terry ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Aston Villa, na Branislav Ivanovic akiwa pale Zenit St.Petersburg kocha Antonio Conte anaukumbuka mchango wao na amepata njia mbadala ya kusuluhisha tatizo ilo la timu kucheza bila wakongwe.

"Ni ngumu kuiongoza timu bila wao (Mikel, Terry na Ivanovic) lakini nadhani ni wakati rasmi wa nafasi zao kuchukuliwa na makinda katika kuweka mambo sawa"

"ni ngumu kumwamini mchezaji ambaye hana udhoufu ukamweka nafasi ya mtu aliye mzoefu ila nadhani kila mtu anataka mafanikio tena mafanikio kwa muda mfupi lakini kwa hali ilivyo sasa inabidi tuwatumie sana makinda ili kuweza kutengeneza udhoefu kwao na tupate mafanikio zaidi ya baadae"

Mpaka sasa makinda kama Ethan Ampadu mwenye miaka 17, Andreas Christensen mwenye miaka 21 na Tiemoue Bakayoko mwenye miaka 23 wanaonekana kutumika zaidi na kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza ambapo kwa mujibu wa kocha Antonio Conte anaona wanaweza kufanya makubwa na kuleta matokeo mazuri.

Kamusi; Serengeti Boys-wachezaji makinda, jina hilo linatumiwa na timu ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya miaka 18

No comments:

Post a Comment