ASENSIO AMZUIA HAZARD KUTUA CHELSEA - Darajani 1905

ASENSIO AMZUIA HAZARD KUTUA CHELSEA

Share This

Klabu ya Real Madrid inaripotiwa na gazeti la nchini Hispania kuwa imesitisha mpango wake wa kumsajili nyota na winga wa Chelsea, Eden Hazard mara baada ya kupata tishio kutoka kwa nyota wake Marco Asensio.

Marco Asensio ameizuia bodi ya mabingwa hao wa Hispania kuendelea na mpango wake wa kumsajili Hazard mara baada ya kutishia kwa kusema kama akisajiliwa Hazard basi naye anaondoka klabuni hapo.

Ambapo kwa kauli hiyo imewazuia mabingwa hao kuendelea na mpango wake wa kumsajili mbelgiji, Hazard.

Asensio amekuwa na kiwango bora klabuni Madrid akiichezea michezo 37 huku akiifungia magoli 7 na ukilinganisha umri wake ambapo kwa sasa ana miaka 21 wakati Eden Hazard ana miaka 26 ambapo kwa hayo umeifanya Real au Los Blancos isitishe mpango huku kuliwai kuripotiwa kuwa klabu hiyo iliandaa paundi milioni 120 ili kumsajili nyota ikiwa ni kianzio chao.

No comments:

Post a Comment