CONTE AKILI YAKE KWA VIDAL - Darajani 1905

CONTE AKILI YAKE KWA VIDAL

Share This
Kuna uwezekano mkubwa Chelsea ikafanya haraka kumsajili mchezaji nyota wa klabu ya Bayern Munich ambaye ni raia wa Chile, Arturo Vidal kutokana na kocha huyo kuonekana ana hamu sana kuungana tena na nyota huyo ambaye walishawai kuwa wote klabuni Juventus ambapo Conte alikuwa kama kocha.

Conte anaonekana kuwa na mapenzi makubwa na nyota huyo ambaye anamaliza mkataba na klabu ya Bayern mwezi wa sita mwaka 2019 na huku akionekana hana mazungumzo mazuri na klabu yake hiyo hali inayoonyesha inaweza kuchochea kwa kisai kikubwa kwa nyota huyo kuunganana kocha wake huyo.

Ambapo katika mkutano mmoja amekaririwa akisema "Hakika Vidal ni mmoja kati ya wachezaji bora duniani" ambapo imeonyesha wazi kuwa kocha huyo anatamani kuungana na nyota huyo.

Arturo Vidal mwenye miaka 30 inaelezwa amekuwa akifanya mawasiliano na Conte ili aungane na kocha huyo huku Conte akihitaji kuipanga Chelsea ambayo amekuwa akikiri ina kikosi kidogo na anahitaji kuongeza wachezaji wenye uwezo wa kupambana kuelekea mwisho wa msimu huu ili kushindania kulitwaa taji la ligi kuu ambalo Chelsea ndiye bingwa mtetezina taji la ligi ya mabingwa Ulaya ambapo Chelsea imepangwa kumenyana na Barcelona katika hatua ya 16 bora.

No comments:

Post a Comment