MAKINDA WA CHELSEA KUREJEA KUISAIDIA TIMU - Darajani 1905

MAKINDA WA CHELSEA KUREJEA KUISAIDIA TIMU

Share This
Kuna taarifa mpya zimezagaa kuwa Chelsea imepanga kuwarudisha baadhi ya nyota wake ambao wapo kwa mkopo ambao ni makinda. Nyota ambao wanatajwa kurejea Chelsea ni pamoja na Kasey Palmer ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Huddesrfield ianyoshiriki ligi kuu Uingereza pamoja na Ike Ugbo ambaye yeye anatokea Barnsley ya nchini Uingereza.


Kasey Palmer mwenye miaka 21 alianza kuonyesha dalili za kuachana na klabu hiyo mara baada ya kutuma ujumbe katika mtandao wa Instagram akiwaaga mashabiki na nyota wenzake klabuni hapo akiwaambia muda wake wa kuendeleza kipaji chake kwenye klabu nyengine umeshafika.

Kasey aliungana na Chelsea akademi mwaka 2013 na kucheza klabuni hapo mpaka kutolewa kwa mkopo mwaka 2016 na kujiunga na Huddersfield aliyoisaidia kupanda daraja kutoka Championship mpaka Ligi kuu huku akiichezea michezo 29 na kuifungia magoli 4.

Wakati kwa upande wa Ike Ugbo ambaye ni mshambuliaji akiichezea klabu hiyo jumla ya michezo 18 katika ligi daraja la kwanza Uingereza maarufu kama Championship ambapo kwa sasa ana miaka 19.

Ugbo aliungana na Chelsea mwaka 2007 kabla ya kuungana na Barnsley mwaka 2017.

Jana kocha Antonio Conte aliulizwa kuhusu kuwaita makinda waliopo kwa mkopo na alijibu "Sina uhakika katika hilo ukizingatia tuliowatoa kwa mkopo wanapata nafasi ya kucheza huko walipo. Mwezi januari mwaka 2017 tuliwarudishwa Nathan Ake, Kenedy na Musonda lakini kwa msimu huu sina uhakika"

Huenda huu ukawa mwanzo mzuri kwa nyota hao katika kujenga viwango vyao maana watakabiliana na michezo migumu ya mzunguko wa pili ambao huwa na michezo migumu.

No comments:

Post a Comment