Kuna taarifa katika mitandao mingi barani Ulaya zimesambaa zikitoka katika gazeti moja la nchini Hispania ambapo kunapatikana klabu ya Real Madrid zikidai kocha wa klabu hiyo, Zinedine Zidane ameagiza wasajiliwe nyota wa klabu ya Chelsea, Eden Hazard pamoja na N'Golo Kante ambapo anadai anawahitaji ili kuirudisha Madrid kwenye moto wake.
Zinedine Zidane amekuwa akitajwa kuvutiwa zaidi na Eden Hazard na amekuwa akimfukuzia kwa muda mrefu huku pia akimuhitaji N'Golo Kante ambaye alikuwa mchezaji bora wa ligi kuu Uingereza msimu uliopita na hata kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ufaransa akiwapiku Karim Benzema wa Madrid na Kylian Mbappe wa PSG.
Lakini taarifa hizo zikaelezea kuwa mmiliki wa klabu hiyo,
Fiorentino Perez hana mpango na ushaurihuo au mapendekezo hayo
yaliyotolewa na kocha wa klabu yake.
ZIDANE AAGIZA HAZARD NA KANTE WATUE MADRID
Share This
Tags
# Chelsea Usajili
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Usajili
Labels:
Chelsea Usajili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment