Klabu ya Chelsea leo imekamilisha uhamisho wa nyota kinda kutoka nchini Austria mwenye asili ya Guinea barani Afrika, Thierno Bello mwenye miaka 16 huku akifanya vizuri akiwa na timu ya taifa ya Austria chini ya miaka 17.
Bello ambaye ni mshambuliaji amekuwa na sifa kubwa huku akiwai kucheza kwenye akademi kadhaa barani Ulaya na kuonyesha kiwango kikubwa huku moja ya akademi alizowai kuzichezea ni akademi ya klabu ya Bayer Leverkusen.
Bello katika maisha yake ya soka aliwai kufunga magoli 200 ndani ya miaka miwili katika moja ya akademi alizokuwa pindi akiwa mdogo.
Karibu Chelsea, labda utaweza kuvivaa viatu vya Didier Drogba na kuwa shujaa kama yeye!
No comments:
Post a Comment