NYOTA WA WIKI; KUMBE WILLIAN ALILETWA KWA NDEGE YA TOTTENHAM? - Darajani 1905

NYOTA WA WIKI; KUMBE WILLIAN ALILETWA KWA NDEGE YA TOTTENHAM?

Share This
Nyota wetu wa wiki ni Willian da Silva Borges, na tumemchagua kuwa nyota wetu wa wiki mara baada ya kuchaguliwa kuwa nyota wa mchhezo dhidi ya Stokecity akiiongoza vyema Chelsea kuibamiza klabu hiyo magoli 5-0.

Nimekuletea makala hii kuhusu nyota huyu kwa mambo ambayo labda huuwai kuyasikia kutoka kwake, au kama uliwai kuyasikia basi hukuwai kupataufafanuzi na utamu zaidi kuhusu jambo hilo au labda hukuwai kulisikia kabisa.

Leo nataka nikurudishe nyuma kidogo mpaka pale ilipotangazwa rasmi kuwa Willian ni mchezaji halali wa Chelsea akisajiliwa kwa dau la paundi milioni 30 akitokea klabu ya Anzhi Machakchala, unakumbua nini kuhusu usajili wake? Najua wengi mtakuw mmekumbukia lile tifutifu lililotokea mara baada ya nyota huyo kusaini Darajani wakati kulikuwa na taarifa kuwa alikuwa akifanyiwa vipimo na Tottenham ili ajiunge na klabu hiyo, lakini baadae kukatokea taarifa kuwa Chelsea imeipiku Tottenham na kufanikiwa kumsajili nyota huyo raia wa Brazil.

Bila shaka unakumbuka tukio lilivyokuwa na kama hukuwai kuipata habari hii, nipo tayari kukujuza kuhusu hali ilivyokuwa.

Ilikuwa mwezi Agosti mwaka 2013 wakati dirisha la usajili likiwa limechachamaa klabu zikifanya usajili kujiandaa na msimu mpya wa 2013/2014. Kulikuwa na tetesi nyingi lakini mojawapo ilimhusu kijana Willian ambaye kwa kipinsi icho alikuwa na miaka 25 akihusishwa kutakiwa na klabu kadhaa za nchini Uingereza ambapo Chelsea, Tottenham na Liverpool zilikuwa zikitajwa kumuwania.

Lakini ikaonekana kama Tottenham au unaweza kuwaita Spurs walikuwa wanaongoza katika kumuwania, na kweli kukazagaa taarifa kuwa Willian karibuni kusainiwa na wababe hao wanaopatikana jiji moja na Chelsea yaani jiji la London. Mara baada ya kiungo au winga huyo kusafiri kutoka klabu yake ya Anzhi yenye makao nchini Urusi akatua katika jiji la London na kufanyiwa vipimo klabuni hapo kabla ya wajanja wa Chelsea kufanya umafia.

Umafia walioufanya wakati Willian akiwa klabuni Tottenham akifanyiwa vipimo, viongozi wa bodi ya Chelsea hawakuataka kuangaika na mchezaji, wao walifanya mawasiliano ya haraka na watu wa karibu akiwemo wakala wa nyota huyo na kukubaliana naye kisha Willian alipomaliza kufanya vipimo na Tottenham akasafiri haraka mpaka Chelsea, na klabu hiyo kumtangaza kuwa mchezaji wao huku Tottenham wakibaki bila kuelewa kitu.

Mwisho wa siku Willian akasaini rasmi Chelsea kwa dau la paundi milioni 30 na kupewa mkataba wa miaka mitano klabuni hapo na kuwaacha viongozi wa Tottenham wakilalamika kuwa wameibiwa.

Baada ya usajili huo, Willian alipohojiwa alisema "Miaka miwili iliyopita nikiwa Shakter Donetsk, Chelsea iliwai kuleta maombi ya kunisajili, ila klabu iligoma kuniuza., lakini nilipendezwa kuja Chelsea. Nimekuwa nikitakiwa na Chelsea, na walipoleta ofa ya kunitaka sikutaka kufikiria mara mbili kukubali maana moyo wangu tayari ulishakuwa Chelsea"

Baada ya usajili huo kukamilika mashabiki wengi wa Chelsea walikuwa wakiandika mabango na kuimba nyimbo kuwatambia au kuwaringishia mashabiki wa Tottenham huku wakiimba kwa kusema "Alipanda ndege ya Tottenham, ila alipopata simu ya tajiri Abramovich akasaini Chelsea"

***Nadhani umepata kitu hapa, kuna wachezaji wanacheza Chelsea ila hawachezi tu kama wachezaji, ila pia kwa vile ni mashabiki. Hongera sana Willian na endelea kupeperusha bendera ya Chelsea maana tunasema KEEP THE BLUE FLAG, FLYING HIGH

No comments:

Post a Comment