Lampard awataja viungo wagumu aliowai kupambana nao - Darajani 1905

Lampard awataja viungo wagumu aliowai kupambana nao

Share This

Alicheza klabuni Chelsea kwa miaka 13 ambapo alisajiliwa akitokea klabu ya West Ham united na sasa anafanya kazi ya uchambuzi wa michezo kwenye chaneli ya BT Sport huku kwa sasa akiendelea kupitia mafunzo ya ukocha wa mchezo wa soka. Huyo ni Frank Lampard ambaye ni gwiji wa Chelsea ambaye ametengeneza rekodi nyingi klabuni hapo huku kubwa zaidi ikiwa ni ile ya kuwa mfungaji bora wa muda wote klabuni Chelsea.

Gwiji huyo amewataja viungo ambao katika maisha yake yote ya soka alikuwa akipata tabu pale anaposhuka uwanjani kucheza dhidi yao.

Nyota huyo amewataja viungo Roy Keane (Man utd), Steven Gerrard (Liverpool), Yaya Toure (Man city), Paul Scholes (Man utd) na Patrick Vieira (Arsenal).

Gwiji huyo raia wa Uingereza anadai kiungo mgumu zaidi ni mwingereza mwenzake, Steven Gerrard huku anayekaribia kumkaribia kwenye ugumu ni kiungo raia wa Ivory Coast, Yaya Toure.

No comments:

Post a Comment