CHELSEA YAPATA USHINDI KWA REKODI HUKO LONDON - Darajani 1905

CHELSEA YAPATA USHINDI KWA REKODI HUKO LONDON

Share This
Wiki tatu zilipita toka kikosi cha vijana cha Chelsea kutoka nje kwenda kucheza mchezo wake wa ligi kuu Uingereza kwa vijana ambapo mchezo wa mwisho, Chelsea ilisafiri na kwenda kumenyana dhidi ya Manchester united na kuishuhudia Chelsea ikipata ushindi wa mabao 4-0, na jana tena ilisafiri na kutoka nje ili kucheza dhidi ya West Ham mashariki mwa jiji la Londdon.

Chelsea ilisafiri mpaka kwenye kiwanja hicho cha Victoria Road na kumenyana na vijana hao wa London. Chelsea ikafanikiwa kuondoka na alama tatu katika mchezo huo ikishinda mchezo kwa goli moja lililofungwa na nyota wa klabu hiyo, Harvey St Clair ambaye alifunga goli hilo dakika ya 19 na kuifanya Chelseaishinde ushindi wake wa nne kati ya michezo mitano iliyopita.

kwa matokeo hayo, Chelsea inashika nafasi ya sita katika msimamo wa ligi kuu kwa vijana hao huku jumatano itakuwa safarini kusafiri mpaka kwenye jiji la Madrid ili kucheza mchezo wake wa robo fainali ya klabu bingwa kwa vijana dhidi ya Real Madrid.



No comments:

Post a Comment