Chelsea ilishuka uwanjani dhidi ya Crystal Palace na kupata ushindi wa mabao 2-1 mwisho wa wiki iliyopita, ushindi ambao unaifanya kufikisha alama 56 katika msimamo wa ligi kuu Uingereza. Kuna maswali mengi yaliibuka katika mchezo, haswa mara baada ya mchezo huo kuisha. Lakini swali mojawapo ambalo liliwaumiza wengi vichwa ni je nani anastahili kutumika kama mshambuliaji chaguo la kwanza katika kikosi cha Chelsea kati ya Olivier Giroud na Alvaro Morata?
Katika mchezo huo, Olivier Giroud ndiye aliyeanza na kutumika kama mshambuliaji chaguo la kwanza, alionekana kwenda sawa na kasi ya mchezo huku akihusika katika mashambulizi mengi, alipata nafasi kadhaa ambazo nafasi kubwa mbili alizozipata moja iliokolewa katika mstari wa goli na mlinzi wa Crystal Palace ambapo mpira ulikuwa unaelekea golini, lakini pia nafai nyengine alipiga vizuri kabla mpira kugonga mwamba na kushinda kuingia nyavuni. Kila shabiki alipendezwa na kiwango chake katika mchezo huo, lakini je ataweza kuendelea na moto huo aliokuwa nao na kutumainika na kocha kutumika kama mshambuliaji wakati chaguo la kwanza? Mpaka sasa ameshaichezea michezo 4 huku akifunga goli moja.
Alvaro Morata amekuwa na kiwango kisichorizisha kwa sasa, toka kuingia mwaka 2018 hajafanikiwa kufunga. Inaonekana jambo kubwa kwake kwa sasa ni kupambana ili kurudia ubora wake alioanza nao klabuni hapa, mashabiki na kocha wa Chelsea, Antonio Conte wote wanaonekana bado kuwa na imani nae na wanatamani kumuona akirudia moto wake ingawa inavyoonekana yeye alipo na ubora anatotaka kuufikia inaoenekana ni njia ndefu bado. Mpaka sasa ameshafunga magoli 12 na kutengeneza mengine matano katika michezo 36. Je Antonio Conte anastahili kumtumia kama mshambuliaji chaguo la kwanza kama ilivyokuwa mwanzo? au ampumzishe mhispania huyu ili apate uchungu wa kupambana zaidi ili kurudia ubora wake kama wanavyosema mashabiki wengi?
Kocha Antonio Conte alihojiwa juu ya mtazamo wake katika mhezo huo, naye alisema "Tumeruhusu kufungwa katika ushindi wa 2-1, mwishoni mwa mchezo kulikuwa na hali kubwa ya kimchezo lakini tulifanya vyema kutoruhusu mpira kuchezewa kwenye eneo letu. Nadhani tulistahili kupata ushindi, tulicheza mchezo mzuri, haswa katika kipindi cha kwanza. Crystal ni timu nzuri haswa inapambana kutokushuka daraja"
"Sasa inatakiwa tujiandae kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Barcelona, ni yimu imara, mchezo utakuwa tofauti kabisa na uliokuwa katika mchezo wa kwanza, lakini pia tuna siku tatu za kujiandaa na kujua ni wachezaji gani wa kucheza kwenye mchezo huo" alisema Antonio Conte.
Hapa nimekuwekea maoni ya mashabiki wa Chelsea walichokieleza juu ya washambuliaji hao wawili, je ni nani anastahili kutumika kama mshambuliaji chaguo la kwanza.

GIROUD AU MORATA NANI KUWA NAMBA MOJA? CONTE ATOA NENO
Share This
Tags
# Chelsea FC
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea FC,
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment