'BATSMAN' AIBEBA TENA DORTMUND - Darajani 1905

'BATSMAN' AIBEBA TENA DORTMUND

Share This
Ulikuwa ni usiku mwengine mtamu kwa mhabiki wa Chelsea mara baada ya kumuona nyota wao akiendeleza moto huko alipo, lakini ilikuwa ni usiku mtamu zaidi kwa mashabiki wa Borrusia Dortmund mara baada ya kuishuhudia klabu yao ikipata ushindi muhimu huku nyota wa Chelsea anayeichezea klabu hiyo kwa mkopo, Michy Batshuayi akiibuka kama shujaa kwa kuipatia ushindi huo muhimu klabu hiyo.

Magoli ya Batshuayi yaliifanya Dortmund iondoke na ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Eintracht Frankfurt katika mchezo wa ligi kuu nchinimUjerumani.

Mchezo huo ulianza huku klabu hizo zikiwa zimelingana alama katika msimamo wa ligi kuu, na Dortmund iliyokuwa nyumbani ilitakiwa ishinde ili ijiweke katika nafasi nzuri. Marco Reus wa Dortmund ndiye alikuwa wa kwanza kufunga na kuifanya timu yake iongoze. Ndipo wapinzani wakachomoa,. Kama kawaida yake, Michy Batshuayi hakutaka kuleta dharau akiwa kazini, akaongeza goli la pili ndipo wapinzani wakachomoa goli hilo katika dakika za majeruhi na matokeo kuwa 2-2.

Dakika za majeruhi kabisa, zikiwa zimebaki dakika kadhaa mpira kuisha, ndipo Batshuayi akaifungia goli la tatu na la ushindi kwa klabu hiyo na kuifanya itambe ikiwa nyumbani. Kwa magoli hayo, nyota huyo anafikisha magoli 7 katika michezo 9 toka ajiunge na klabu hiyo mwezi Januari.

Hongera Michy Batshuayi  'Batsman'

No comments:

Post a Comment