Chelsea inapata ushindi wake muhimu katika mchezo wa ligi kuu Uingereza dhidi ya Crystal Palace, ambapo magoli ya Chelsea yakifungwa na winga wake matata, Willian Borges da Silva pamoja na jengine mlinzi wa Crystal, Kelly akijifunga mara baada ya Chelsea kufanya shambulizi la hatari lililowazubaisha walinzi wa Crystal palace.
Kwa matokeo hayo ya 2-1, Chelsea inarudi katika hali yake ya ushindi kabla ya jumatano hii kumenyana dhidi ya Barcelona katika mchezo wa klabu bingwa barani Ulaya ambapo itasafiri mpaka nchini Hispania kumenyana dhidi ya Barcelona.
Kama ulikosa kuutazama mchezo dhidi ya Crystal Palace, basi nimekuwekea video hapa.
Habari, jina langu ni Barnabas Gwakisa ni kijana raia wa Tanzania ninayeshabikia klabu ya Chelsea na ninakuletea ukurasa huu ili upate habari zote kuhusu Chelsea FC, Chelsea FC Women (kwa wanawake) na Chelsea Youth (kwa vijana wa akademi), Asante,....Read More ?
No comments:
Post a Comment