KENNEDY NAYE AWA NYOTA HUKO Newcastle - Darajani 1905

KENNEDY NAYE AWA NYOTA HUKO Newcastle

Share This

Jana wakati Chelsea ilipokuwa inashangilia miaka 113 toka kuundwa kwake tarehe 10-Marchi-1905, nyota wa klabu hiyo anayeichezea klabu ya Newcastle, Kennedy Robert naye alikuwa anashangilia kufunga goli lake la kwanza akiichezea klabu hiyo ya Newcastle huku akifunga mara mbili katika mchezo wa ligi kuu ambapo Newcastle ilikuwa uwanjani kumenyana dhidi ya Southampton na kuisaidia klabu yake kupata ushindi wa mabao 3-0.

Kennedy ambaye ni nyota wa Chelsea anayeicheza klabu hiyo kwa mkopo mara baada ya kujiunga nayo katika dirisha dogo la usajili la mwezi wa Januari, aliiongoza vyema klabu ya Newcastle na kuisaidia kupata ushindi huo mnono uliowasogeza kwenye msimamo wa ligi hiyo mpaka nafasi ya 13. Kumbuka pia timu hiyo inaongozwa na kocha wa zamani wa Chelsea ambaye aliisaidia Chelsea kushinda taji la Europa mwaka 2013, Rafa Benitez.

Na kupitia mtandao wa Instagram, nyota huyo alituma ujumbe kuonyesha kwa kiasi gani alivyofanikiwa kufikia mafanikio hayo.

Hongera Kennedy Robert.

No comments:

Post a Comment