CHELSEA KUMPOTEZA NYOTA WAKE - Darajani 1905

CHELSEA KUMPOTEZA NYOTA WAKE

Share This

Kuna wachezaji ambao wamesajiliwa kwenye timu lakini wakaishia kutolewa kwa mkopo bila hata kuichezea klabu yao mchezo wowote unaotambulika, moja kati ya wachezaji hao ni nyota wa Chelsea, Matec Delaj ambaye inaripotiwa ana mpango wa kuachana na Chelsea na kutafuta klabu nyengine ifikapo mwisho wa msimu huu.

Matec alijiunga na Chelsea mwaka 2009 lakini hajafanikiwa kuichezea Chelsea mchezo wowote unaotambulika huku akiishia kutolewa kwa mkopo.

Nyota huyo mwenye miaka 25 anayecheza nafasi ya mlinda mlango mwaka jana alihojiwa kama atasaini mkataba mpya huku mkataba wake wa sasa ukiwa unaisha mwezi Juni mwaka huu, amesema
"Ndiyo, naamini itafika muda wa mimi kuondoka Chelsea" alisema nyota huyo.

Alipoulizwa kama anajuta kufika Chelsea huku akiwa kijana wa umri mdogo na kushindwa kuichezea mchezo wowote maalumu, nyota huyo alisema "Hapana sijutii, wengi wamekuwa wakizani hivyo lakini kiukweli mi nipo sawa"

No comments:

Post a Comment