Leo ni siku ya kuzaliwa ya gwiji wa Chelsea, Didier Drogba ambaye anatimiza miaka 40 toka kuzaliwa kwake mwaka 1978 huko nchini Ivory Coast, nasi kama Darajani 1905 ni lazima tuonyeshe kwa kiasi gani tunafurahishwa na siku muhimu kama hii kwa nyota huyu.
Lakini kutokana na ukongwe wake na ukubwa wake katika soka la Afrika na hata soka la barani Ulaya haswa klabuni Chelsea hatupendezwi kama siku muhimu ya mchezaji huyo ikapita bila kutoa pongezi zetu kwake.
Amefanya mengi klabuni Chelsea, amefanya mengi makubwa katika soka la barani Ulaya, amefanya mengi makubwa katika soka la Afrika na hata katika soka la dunia. Mengi makubwa. Ambapo sidhani kama kuna haja ya kueleza yapi haswa aliyoyafanya lakini bila shaka kila anayemfahamu anajua ni yapi kayafanya.
Anakumbukwa haswa na mashabiki wa Chelsea katika ule mchezo wa fainali ya klabu ya mabingwa Ulaya dhidi ya bayern Munich katika uwanja wa Allianz Arena akiwa anaenda kupiga mkwaju wa penati wa mwisho na kuipatia Chelsea taji lake la kwanza la klabu bingwa barani Ulaya, taji la kwanza la Ulaya lililoifanya Chelsea kuwa klabu ya kwanza jijini London kubeba taji hilo la Ulaya.
Kuna mengi kayafanya ambayo hakuna mtu asiyeyajua, huku wengi wakiamini ndiye mshambuliaji hatari kuwai kutokea klabuni Chelsea.
Kupitia mtandao wa Instagram, nyota huyo ambaye kwa sasa ni mmoja wa wamiliki wa klabu ya Phoenix ya nchini Marekani, alituma ujumbe ulioonganishwa na video ili kuwashukuru wote waliomtakia heri na fanaka katika siku yake ya kuzaliwa.
Hongera Didier Drogba, ni lazima tukutakie heri hii mfalme wa soka...

HERI YA KUZALIWA DIDIER DROGBA
Share This
Tags
# Chelsea FC
# Chelsea Habari
# Mitandaoni
Share This
About Darajani 1905
Mitandaoni
Labels:
Chelsea FC,
Chelsea Habari,
Mitandaoni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment