PL; Ft, CHELSEA 2-1 Crystal Palace - Darajani 1905

PL; Ft, CHELSEA 2-1 Crystal Palace

Share This

Chelsea wanapata ushindi muhimu ambao unaipatia alama tatu zinazoifanya ifikishe alama 56 kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza huku ikiwa nafasi ya tano, ikiachwa alama mbili na Tottenham inayoshika nafasi ya nne.

Willian ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuifungia Chelsea, akifunga goli la kuongoza kwa kupiga shuti akiwa nje ya eneo la hatari na kuifanya Chelsea kuwa mbele katika kipindi cha kwanza. Dakika kadhaa baadae, Chelsea ilitengeneza shambulizi ambapo Marcos Alonso aliumiliki mpira kabla ya kutoa pasi ya kuburuzika akiitoa ndani ya eneo la 18 lakini Willian akaukwepa mpira na kumwachia Eden Hazard ambaye naye kwa ustadi akamtengea Zappacosta aliyepiga shuti na kuzuiliwa ila bado mpira ulikuwa kwenye kasi na kujikuta mlinzi wa Crystal akijifunga na kuifanya Chelsea kuwa mbele kwa ushindi wa mabao 2-0 mpaka mpira kwenda mapumziko.

Kipindi cha pili, Chelsea iliendelea kufanya mashambulizi ambayo kama wamaliziaji wangekuwa makini basi Chelsea ingeondoka na ushindi mnono.

Mabadiliko yakafanyika, Giroud akatoka na nafasi yake kuchukuliwa na Morata, Eden Hazard nafasi yake kuchukuliwa na Tiemoue Bakayoko huku Fabregas akitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Pedro.

Mara baada ya mabadiliko hayo, Crystal Palace ikaonekana kuanza kuutawala mchezo huku ikitengeneza mashambulizi mengi zaidi mpaka kufanikiwa kupata goli moja lililofungwa na Van Aanlot ambaye alishawai kuichezea Chelsea. Na kufanya mpaka mpira unaisha, Chelsea 2-1 Crystal Palace

Sasa Chelsea inajiandaa kusafiri ili kwenda nchini Hispania kumenyana dhidi ya Barcelona katika mchezo wa raundi ya 16 bora, mchezo huo utachezwa jumatano ya tarehe 14-Marchi.

No comments:

Post a Comment