Katika mchezo wa jana ambao Chelsea ilimenyana dhidi ya Afc Bournemouth, nyota mpya wa Chelsea, Olivier Giroud alikuwa jukwaani akiushuhudia mchezo huo akiwa sambamba na nyota mpya mwengine Emerson Palmieri ambaye alisajiliwa akitokea klabu ya As Roma ya nchini Italia.
Nyota huyo Giroud amesajiliwa akitokewa klabu ya Arsenyani (Arsenal) kwa dau la paundi milioni 18 na kupewa mkataba mwa mwaka mmoja na nusu.
Gwiji wa soka ambaye alikuwa mchezaji wa Arsenyani, Thierry Henry ametoa neno juu ya usajili wa mfaransa mwenzake kutua klabuni Chelsea katika dirisha lililofungwa jana usiku.
"Ni jambo la huzuni sana kumuona Giroud akiwa na jezi ya bluu (jezi za Chelsea) japo itakuwa ni sawa amevaa jezi ya Ufaransa lakini alishazoeleka kuwa na jezi nyekundu zenye michirizi meupe (jezi za Arsenyani)"
"Naamini amekuwa na muda mzuri klabuni Arsenal, na amekuwa akionyesha kupambana kila muda tangu alipokuwa pale. Sitegemii kusikia maneno mabaya kutoka kwa shabiki wa Arsenal juu yake" alisema mkongwe huyo wa Arsenyani.
No comments:
Post a Comment