Chelsea imepoteza mchezo wake muhimu hapo jana ilipocheza dhidi ya Afc Bournemouth ambapo kama ingeshinda mchezo huo ingekuwa imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kufanikiwa kufuzu kucheza michuano ya klabu bingwa Ulaya kwa msimu ujao.
Mara baada ya mchezo huo, kocha Antonio Conte alifanya mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia machache kuhusu mchezo huo na nini kinaendelea klabuni Chelsea, na hapa nakuletea kwa ufupi aliyoyazungumza.
Alipoulizwa sababu ya kupoteza mchezo huo na kuulizwa kama huenda kuumia kwa mlinzi Andreas Christensen na kuondoka kwa Michy Batshuayi muda mfupi kabla ya mchezo alisema "Hapana, hakuna sababu katika kupoteza mchezo huo maana ata Christensen alishawai kutotumika na hata Cahill kucheza katikati na bado tulipata ushindi na hatukuruhusu kufungwa na hata huyo Batshuyi huwezi kutumia kama kisingizio cha kupoteza mchezo wa leo. Kumbuka kabla hata ya mchezo nilisema kabla kuwa mchezo huu ni mgumu sana japo watu wanautazama kiurahisi. Tutajaribu kutafuta visingizio vingi kwa kupoteza mchezo huu lakini naamini mchezo ulikuwa mgumu. Na kama tukishinda huwa tunashinda wote kama timu basi hata kupoteza inabidi tupoteze wote"
Alipoulizwa juu ya majeruhi ya Andreas Christensen aliyeumia kipindi cha kwanza na nafasi yake kuchukuliwa na Antonio Rudiger, kocha alisema "Kuhusu hilo kwa sasa sijajua, labda muhimu tusubiri siku ya leo ipite kisha tupokee taarifa kutoka kwa daktari"
Alipoulizwa juu ya nafasi ya Chelsea kutetea taji lake la ligi kuu huku ikiachwa alama 15 na vinara wa ligi kuu Mama site (Man city), kocha huyo alijibu "Toka kuanza kwa msimu nilisema msimu huu utakuwa mgumu sana, na mpaka kufikia hapa tulipo nadhani malengo makubwa ya klabu mpaka sasa sio tena kutetea taji la ligi kuu, ila kupata nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya kwa msimu ujao yatakuwa ni mafanikio makubwa sana kwetu"
Alipoulizwa juu ya mahusiano yake na timu kwa sasa alisema "Mimi pamoja na makocha wenzangu tunafanya kazi kubwa sana kupambana katika kipindi hiki, na hata hilo najaribu kuliamisha kwa wachezaji, na tumekuwa tukipambana kwa pamoja kwa asilimia zaidi ya 120. Na katika hili naamini sasa wachezaji watakuwa wanaona kuwa tuna msimu mgumu kwa hiyo kupambana itakuwa zaidi sana kuliko msimu uliopita"
Hayo ndio baadhi aliyoyaongea kocha huyo katika mchezo wa jana, je una maoni gani katika hayo?
No comments:
Post a Comment