Ni usiku mgumu na mbovu kwa kila shabiki wa Chelsea popote alipo mara baada ya kupokea kipigo kutoka kwa klabu inayoshika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza.
Kipindi cha kwanza kilianza kwa Chelsea kumiliki mpira vizuri huku ikicheza kwa mara nyengine bila kuwa na mshambuliaji wa kati ambapo Alvaro Morata ni majeruhi wakati Michy Batshuayi akiwa amekamilisha uhamisho wa kuungana na Borrusia Dortmund ya nchini Ujerumani.
Mpaka mpira unaenda mapumziko, matokeo yalikuwa 0-0 huku Chelsea akiwa hana uhiano mzuri wa kupiga mashuti langoni mwa Bournemouth na kipindi cha pili ndicho kilikuwa kipindi kigumu kuamini kwa kila shabiki wa Chelsea mara baada ya kushtukiza magoli ya harakaharaka na kuifanya Chelsea ipoteze mchezo wake wa kwanza kati ya michezo nane ambayo ilicheza bila kupoteza alama zote tatu.
Waliocheza chini ya kiwango:
Gazeti la Dailystar limewataja nyota wa Chelsea ambao leo wamecheza chini ya kiwango ambao ni Gary Cahill, Antonio Rudiger, Tiemoue Bakayoko na Ross Barkley ambaye ametoka majeruhi na anaonekana bado hajawa sawa kuendana na mbinu za kocha.

No comments:
Post a Comment