Kuna taarifa mpya zimetoka zikitoka kwenye moja ya vyombo vya habari vinavyoaminika zikisema Chelsea imeamua kuachana na mpango wake wa kuwasajili nyota wawili kutoka klabuni As Roma ambao ni Edin Dzeko na Emerson Palmieri ambao wote kwa ujumla walikuwa wanaigharimu Chelsea kuwapata nyota hao.
Dili la Dzeko linatajwa kuvunjika kutokana na nyota huyo kutaka mkataba wa mpaka mwezi juni mwaka 2022 ambapo kwa sasa ana miaka 31 na siku kadhaa kutimiza miaka 32. Wakati kwa upande wa Chelsea wenyewe wapo tayari kumpa mkataba mpaka mwaka 2019.
Lakini pia mara baada ya kuachana na nyota huyo ikaelezwa pia nyota mwengine klabuni hapo aliyekuwa anatajwa kutakiwa na Chelsea, Emerson Palmieri nae ameachwa na Chelsea huku sababu kubwa ikitajwa Chelsea kutokuwa tayari kutoa fungu la kumsajili nyota huyo wakati akiwa amekuwa muda mrefu akiuguza majeraha kwa miezi sita na toka amerudi hana uhakika.
No comments:
Post a Comment