Bodi ya klabu ya Chelsea inatajwa kumpiga marufuku kocha wa klabu hiyo, Antonio Conte mara baada ya kocha huyo kusema hana mamlaka ya kufanya usajili mahali hapo ambapo alisema maneno hayo juzi mara baada ya mchezo wa nusu fainali ya kombe la ligi ambapo Chelsea ilikuwa ugenini kupambana dhidi ya Arsenyani (Arsenal) ambapo mchezo huo uliisha kwa Chelsea kupoteza kwa kufungwa magoli 2-1.
Mara baada ya mchezo huo kocha Conte alihojiwa na waandishi wa habari na kulalamika kuwa ana sauti ndogo katika swala la usajili klabuni hapo huku akitoa mfano mara baada ya kuumia kwa Willian katika mchezo huo kulikuwa na mchezaji mmoja tu aliyebenchi angeweza kuingia kuchukua nafasi ya nyota huyo ambaye ni Ross Barkley, ambapo kwa kauli hiyo inatafsiriwa kuwa pia anahitaji wachezaji zaidi ila bodi ya klabu hiyo haijali kuhusu anachokisema.
Bodi ya ligi inayoongozwa na mwanamama, Marina Glanovskaia mpaka sasa imeshakamilisha usajili wa nyota mmoja, Ross Barkley toka kuondoka kwa Michael Emenalo huku bodi hiyo ikihusishwa kwa karibu kuwanasa Edin Dzeko na Emerson Palmieri ambao wote wawili wanatokea klabu ya As Roma.
Je unazani ni kweli bodi ya Chelsea aimtendei haki kocha Antonio Conte?
No comments:
Post a Comment