HAZARD AIKATAA CHELSEA - Darajani 1905

HAZARD AIKATAA CHELSEA

Share This
Nyota wa zamani wa klabu ya Chelsea, Thorgan Hazard ambaye ni mdogo wa nyota wa sasa wa klabu hiyo, Eden Hazard amekataa kurudi Chelsea na kutaka aendelee kuichezea klabu yake ya sasa ambayo anaichezea ya nchini Ujerumani inayoshiriki ligi kuu nchini humo, klabu ya Borrusia Monchnglebach.

Nyota huyo alipohojiwa juu ya fununu za kutakiwa klabuni Chelsea alijibu "Kwa sasa nipo hapa, na ukizingatia bado nna mkataba wa kuendelea kucheza hapa mpaka mwaka 2019 na nadhani mazungumzo yanaweza kuanza muda wowote kuanzia sasa ili kusaini mkataba mpya. Natamani kuendelea kuwa hapa"

Na alipoulizwa kama hatamani kujiunga Chelsea ili akacheze na kaka yake alijibu "Kwanza kwa sasa sina kiwango cha kufanana nae, ila pia najihisi vyema sana kama kucheza kwetu kukiwa kwa kukutana kwenye timu ya taifa" alisema nyota huyo ambaye hakupata muda zaidi wa kucheza ndani ya Chelsea ambapo alisajiliwa mwaka mmoja na kaka yake kabla ya kutolewa kwa mkopo na baadae kuuzwa kabisa klabuni huko.

No comments:

Post a Comment