Nyota wa klabu ya As Roma, Edin Dzeko anatajwa kwa karibu kutakiwa na Chelsea huku dili hilo likiwaumiza kichwa viongozi na bodi ya Chelsea juu ya mahitaji muhimu ya mchezaji huyo ili atue klabuni hapo. Mpaka sasa kumekuwa na taarifa mpya ikitoka kuwa nyota huyo anaweza akatua muda wowote huku jumapili iliyopita ilitolewa taarifa kuwa wakala wa nyota huyo amesafiri kwenda kufanya mazungumzo na Chelsea na ikaelezwa nyota huyo pamoja na mwenzake Emerson Palmieri wote kutoka klabuni As Roma wanaweza kutua Chelsea muda woowte haswa ikitegemewa mpaka jumanne usajili huo ungekuwa umeshakamilika, lakini siku ikafika na hakuna aliyetua.
Unajua chanzo ni nini mpaka nyota huyo inashindikana kutua Chelsea? Sababu ni kwamba nyota huyo kwa sasa ana miaka 31 na anatimiza miaka 32 mwezi Machi, amefanya mazungumzo na Chelsea na kuiambia anataka mkataba mpaka wa mwaka 2020 wakati kwa sheria za Chelsea zinasema hauna mchezaji atakayeibgia klabuni hapo akawa na miaka zaidi ya 30 alafu akapewa mkataba zaidi ya mwaka mmoja.
Kwa maana hiyo, Chelsea inataka kumpa mkataba mpaka wa mwaka 2019 wakati yeye anataka wa miaka miwili au zaidi au kama hilo likishindikana basi Chelsea iwe tayari kumpa mshahara mnono zaidi.
Wakati kwa Palmieri, Chelsea inaonekana kusuasua juu ya usajili wake kutokana na nyota huyo kutumia muda mwingi kuwa majeruhi kwa hivyo Chelsea inaogopa kutoa la euro milioni 20 ili kumnasa mtu ambaye huenda baada ya kufika chelsea akawa ameshuka kiwango.
chelsea imekuwa ikitajwa kuwatayari kutoa kiasi cha uro milioni 52 ili kuwanasa hao wote wakati kwa mchanganuo ni kama Edin Dzeko ana thamani ya euro milioni 30 na Emerson ni kama ana thamani ya Euro milioni 20 wakati hicho kiasi kinachobaki ni kama bonasi.
EDIN DZEKO AIUMIZA KICHWA CHELSEA
Share This
Tags
# Chelsea Usajili
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Usajili
Labels:
Chelsea Usajili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment